Jumatatu 25 Mei 2026 - 10:30
Makundi ya waombolezaji wa Bahrain yapinga vitisho na vitendo vya kutishia vya viongozi wa Kidini wa Bahrain

Hawza/ Kwa mara nyingine, wananchi wa Bahrain wamethibitisha kuwa ni watu wa wilaya na msimamo thabiti kwa kuandaa misafara na makundi ya maombolezo, hawakujali vitisho na maonyo yaliyotolewa na viongozi wa Bahrain.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kwa mara nyingine wananchi wa Bahrain wamethibitisha kuwa ni watu wa wilaya na uthabiti, katika usiku wa kumbukumbu ya shahada ya Imam Jawad (as), wengi wenye chuki walitarajia kwamba wafuasi wa Ahlul-Bayt (as), baada ya vitendo vya kibaguzi vilivyotekelezwa hivi karibuni, hasa dhidi ya wanazuoni wakubwa na mashuhuri wa Kishia nchini Bahrain, wangesalimu amri mbele ya vitisho na maonyo yaliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bahrain.

Mandhari ya mitaa ya Bahrain katika usiku wa shahada hiyo yalikuwa na athari kubwa na yalibeba ujumbe wa wazi kwamba hakuna mjadala kuhusu utambulisho wa Kiislamu, itikadi, maombolezo, alama za kidini, wala huzuni yetu kwa Maimamu wetu (as) katika kila mnasaba, maandamano haya ya maombolezo na misafara hii ni mfano wa ikhlasi na uaminifu katika njia ya Ahlul-Bayt (as), licha ya changamoto yoyote wanayokabiliana nayo.

Uwepo mkubwa wa wananchi katika vijiji na vitongoji ulitoa jibu tofauti kabisa na lile ambalo mamlaka zilikuwa zikilitaka, watu walijitokeza katika viwanja vya wazi, mitaa ilijaa misafara ya maombolezo, na bendera nyeusi zilipandishwa tena, taswira hii inathibitisha kwamba kumbukumbu ya kidini na ya wananchi wa Bahrain haiwezi kwa namna yoyote kudhibitiwa kwa amri za kiusalama, wala haiwezi kwa urahisi kunyenyekea chini ya mantiki ya hofu.

Katika siku za hivi karibuni, serikali ilijaribu kulazimisha mlinganyo mpya: “Ima maombolezo yawe chini ya udhibiti kamili, au yasifanyike kabisa katika maeneo ya umma na nje ya Husainiya.” Lakini kilichotokea kwa uhalisia kilionesha mipaka ya vikwazo na udhibiti huo, katika maeneo mbalimbali ya Bahrain, misafara na makundi ya maombolezo yalitoka na kutembea mitaani kwa uwepo mkubwa, hasa wa vijana, kana kwamba ilikuwa kura ya maoni ya kimya ya wananchi kuhusu haki yao ya kufanya sherehe na ibada zao za kidini na kuonesha utambulisho wao wa pamoja.

Serikali ambayo ilitaka katika mtihani wake wa kwanza baada ya kuwakamata wanazuoni wa dini kugeuza maombolezo kuwa suala la kiusalama pekee, ilikabiliwa na ukweli kwamba; uwepo wa wananchi una nguvu zaidi kuliko lugha ya hofu na vitisho, tangi mwanzo hali ya mvutano, mazingira ya vitisho, wito wa kufika kwa vyombo vya usalama na ufuatiliaji mkali vilitawala, wakati huo huo taarifa rasmi ilitolewa ikijaribu kuhusisha misafara ya wananchi na madai ya “kuvuruga utulivu wa umma,” Hata hivyo, wananchi wa Bahrain walilishughulikia suala hili kama jambo la uwepo wao na la kidini, si kama tukio la msimu linaloweza kufutwa kwa amri ya kiutawala.

Misafara hii ya hivi karibuni haikuwa tu mikusanyiko ya jadi ya kidini, bali ndani ya maudhui yake ilibeba ujumbe wazi kwamba licha ya juhudi zote za kutisha watu na kuunda mfano wa Shia anayekuwa mwaminifu kwa mamlaka, jamii bado iko hai, picha na video zilizochapishwa zinaonyesha idadi kubwa ya waombolezaji wakitembea kwa kujiamini mitaani na kutokujali mazingira ya vitisho. Uwepo huu wa jumla uliikumbusha tena jamii ukweli kwamba vikundi vya Huseyniya nchini Bahrain si sherehe za muda mfupi tu, bali ni sehemu ya kina na yenye mizizi imara katika fahamu za wananchi na utamaduni wa mahali hapo.

Hata hivyo, kuna mkanganyiko wa wazi katika mazingira ya Bahrain ya leo, Serikali daima huzungumza mazungumzo ya ustaarabu na uwazi, lakini katika uwanja wa vitendo inashughulikia mikusanyiko ya kidini ya wananchi kwa mtazamo wa kiusalama pekee, wakati Wizara ya Mambo ya Ndani inajaribu kujionesha kama taasisi inayosimamia shughuli hizo na kuhifadhi utulivu, wananchi wengi wa Bahrain wanaamini kwamba; lengo halisi ni kuweka mazingira yote ya kidini ya wananchi chini ya uangalizi kamili kwa mtazamo wa kisiasa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha